12 Machi 2025 - 18:26
Source: Parstoday
Iran: Hatuchukui maagizo kutoka kwa yeyote kuhusu teknolojia ya nyuklia

Makamu wa Kwanza wa Rais, Mohammad Reza Aref amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko imara katika sera yake huru ya nyuklia na wala haishauriani au kuchukua maagizo kutoka kwa mtu yeyote yule.

Akihutubia katika hafla ya kuapishwa mkuu mpya wa Taasisi ya Iranolojia hapa mjini Tehran leo Jumanne, Aref  amesema kuwa, "kiini cha ustaarabu wa Iran ni elimu na maarifa, hata katika maeneo ya mbali sana duniani."

Amesema: "Lazima tustafidi vizuri na teknolojia ya hali ya juu zaidi na kuhakikisha teknolojia hizi pamoja na ustaarabu wa Iran unawafaidisha vizuri wengine."

"Lazima tufaidike na teknolojia ya nyuklia kama tunavyofaidika na teknolojia nyinginezo, katika kuwanufaisha wanadamu na kutatua matatizo katika jamii. Hatushauriani wala hatuombi idhini kutoka kwa yeyote katika suala hili na wakati huo huo tunayafanya maendeleo yetu ya teknolojia yawanufaishe watu wote,' ameongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran. 

Amegusia pia kampeni chafu za nchi za Magharibi za kueneza chuki dhidi ya Iran na kusema kuwa, "ustaarabu na utamaduni wa Iran ndiye mkombozi wa ubinadamu kwani hivi sasa umenawirishwa kwa ustaarabu wa Kiislamu na ina ustaarabu tajiri na mkongwe sana. 

Amesema: "Nchi za Magharibi zinapaswa kuzingatia misimamo ya wazi ya Iran katika sera zake ambazo zinaifanya kuwa nchi pekee isiyotaka silaha za nyuklia kwa kufuata amri za kidini zinazoharamisha kumiliki silaha za mauaji ya umati. Tunafuata fatwa ya Kiongozi Muadhamu. Fatwa hiyo inakataza utengenezaji wa silaha za nyuklia na inaidhinisha matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia. Kila kona ya Iran inatekeleza sera hiyo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha